Ufuatiliaji wa Sera na Utendaji wa EAAMO'22

Wito wa Ushiriki

Tarehe ya mwisho: 20 Aprili, 2022, Kokote Duniani

Tarehe: Octoba 6-9, 2022

Kiunga cha Kuwasilishia: EasyChair

Kongamano la pili la Usawa na Ufikiaji katika Mifumo, Taratibu, na Uratibu (EAAMO ‘22) utafanyika mnamo tarehe 6-9 mwezi Oktoba, 2022, mjini Washington, DC, nchini Marekani.

Lengo la tukio hili ni kuangazia kazi ambapo mbinu kutoka kwenye mifumo, taratibu na uratibu wa hesabu za biashara, pamoja na ufahamu kutoka kwenye sayansi ya jamii na masomo ya kibinadamu, inaweza kuboresha ufikiaji wa fursa kwa jamii ambazo hazikustahili kihistoria na jamii zenye shida.

Kongamano hilo linakusudia kukuza jamii anuwai, kuwezesha muingiliano kati ya wasomi, tasnia, na sekta za umma na za hiari. Ili kutekeleza hili, inachukua mtazamo mpana wa namna utafiti unavyoweza kuchangia upatikanaji wa fursa, na unakaribisha kazi kutoka kwenye hatua zote za utafiti kuingia kwenye vitendo. Hii pia inahusisha kazi ambayo inaangazia ufahamu wa kawaida juu ya utendaji kazi wa mifumo ya kijamii. Programu hiyo itaangazia uwasilishaji muhimu kutoka kwa watafiti na watendaji na pia michango ya uwasilishaji katika utafiti, sera na utendaji.

Tunaomba mawasilisho katika ufuatiliaji wa utafiti na ufuatiliaji wa sera na utendaji. Mawasilisho yanaweza kujumuisha utafiti, uchunguzi, na nyaraka za lengo lililotakiwa na pia mawasilisho yanayochagizwa na matatizo na utendaji kutoka kwa wasomi kutoka kwenye nyanja yoyote na watendaji kutoka kwenye sekta yoyote.

Tunahimiza mawasilisho kutoka kwenye taaluma za aina mbalimbali na ukigusia maeneo yanayohusisha ushiriki wa raia, data za uchumi, ubaguzi na upendeleo, ukosefu wa usawa wa kiuchumi, maendeleo ya kiuchumi, elimu, mazingira na hali ya hewa, huduma za afya, nyumba, masoko ya kazi, na sheria na sera. Mawasilisho yatapitiwa na wataalamu wenza katika eneo husika la kitaaluma. Mwisho wa mawasilisho ni tarehe 20 Aprili, 2022.

ACM EAAMO ni sehemu ya mpango wa Kubuni Utaratibu kwa Faida ya Jamii (MD4SG), na unaundwa kwenye mifululizo ya semina za mafunzo ya kiufundi ya MD4SG na semina za ukufunzi kwenye mikutano ikiwa ni pamoja na ACM EC, ACM COMPASS, ACM FAccT, na WINE. and builds on the MD4SG technical [workshop series] and tutorials at conferences including ACM EC, ACM COMPASS, ACM FAccT, and WINE.

Aina za Uwasilishaji

Mawasilisho yatatarajiwa katika moja kati ya vipengele viwili:

Kwa mawasilisho yote katika ufuatiliaji wowote, mada za kuwasilisha zinajumuisha zifuatazo lakini hazizuiliki kwenye:

 • changamoto za muundo wa soko na utaratibu katika mazingira yenye rasilimali chache
 • mifumo ya ugawaji ili kuboresha upatikanaji wa fursa
 • kuboresha utoaji wa huduma za kijamii na tathmini
 • kutenga fedha za bima ya afya na kusimamia upatikanaji wa huduma za afya
 • utoaji sawa wa huduma za afya katika jamii zote
 • ukosefu wa usawa wa kiuchumi na uhamaji wa makazi kizazi na kizazi
 • kupunguza matokeo ya uchumi yasiyolingana katika masoko ya kazi ya kwenye soko na nje ya soko
 • kugundua uwepo au sababu za tabia ya kinyonyaji ya soko katika masoko ya kazi
 • kuboresha utofauti na usawa kwa kutumia njia za kimfumo
 • kanuni za soko kwa ajili ya data na faragha
 • kutathmini athari za walimu, shule, au sera ya elimu
 • kuboresha ugawaji wa rasilimali za kielimu
 • kupima na kutathmini maendeleo kufikia malengo ya maendeleo endelevu
 • kupunguza udororaji katika mashamba ya wakulima wadogo na usimamizi wa usambazaji wa rasilimali duni
 • mapendekezo ya kimfumo kuhimiza ushiriki wa raia
 • kutathmini usawa katika uwakilishi wa uchaguzi
 • kutoa taarifa ya mabadiliko ya hali ya hewa na muundo wa sera
 • kubuni mifumo sawa ya usafirishaji
 • kukabiliana na changamoto za miundombinu zinazoathiri jamii zilizotengwa
 • kuzingatia maadili wakati wa kutumia hatua zinazotaarifiwa na mfumo na muundo wa utaratibu katika mipangilio ya sekta ya umma

Ufuatiliaji wa Sera na Utendaji

Ufuatiliaji wa sera na utendaji umejitolea kwenye mawasilisho kutoka kwa watafiti na wataalam wa eneo ambao wanasisitiza kazi inayotumika, masuala ya sera, au shida za kiutendaji. Watu walio na ushirika wowote wa kitaasisi au shirika wanaweza kuwasilisha ufuatiliaji huu, na tunahimiza sana michango kutoka kwa watu binafsi katika mashirika ya serikali na yasio ya serikali na tasnia kadhaa. Mawasilisho yatatokea katika moja ya maeneo matano ya kuzingatia:

 • Mawasilisho ya hifadhidata ya mambo yanayowezekana ya hifadhidata zilizokusanywa na kuandikishwa kwa madhumuni ya kukuza utafiti mpya katika sehemu kuu tofauti za matumizi, kuunda viwango vipya vya ukusanyaji wa data, uwazi, na uwajibikaji, na kukuza ushirikiano kati ya taaluma mbalimbali. Uwasilishaji unapaswa kujumuisha hifadhidata, ambayo itapakiwa kama faili la ziada na pia taarifa za metadata. Hifadhidata inaweza pia kupakiwa kwenye huduma za nje za kushirikisha data, na mkutano huo utatoa chaguo la ziada kwenye jukwaa la data wakati wa kukubali kuwasilisha. Uwasilishaji unapaswa kuambatana na hati inayoelezea sehemu kuu ya programu, uwezekano wa utumiaji wa data, na masuala yoyote yanayojulikana, mapungufu, na maoni ya kimaadili ya ukusanyaji, uboreshaji, ufikiaji, na matumizi. Waandishi wanahimizwa kuzingatia maswali yaliyowasilishwa kwenye Jedwali la Mapendekezo ya Hifadhidata.

 • Maonesho ambayo yanaweza kuigwa na/au kupelekwa kwenye mifumo ya programu na majukwaa ya mitandaoni. Mawasilisho ya maonesho yanapaswa kuambatana na maelezo ya mfumo na maagizo ya kina ya namna ya kuyatumia. Uwasilishaji huo unapaswa pia kujumuisha hati inayoelezea shida hasa ambayo mfumo unataka kushughulikia, umuhimu wa shida hii, mapungufu yoyote yanayojulikana au changamoto za hiyo au mifumo kama hiyo, mazingatio ya kijamii na maadili ya kutumia mfumo kama huo, na pia uwezekano wa maendeleo ya baadae.

 • Nyaraka za Utendaji ambazo zinawasilisha mfumo na mtazamo wa jambo linalowezekana kufanyika au kufungua eneo jipya la mjadala kuhusu mada fulani inayohusiana na wigo wa mkutano huo. Tunahimiza mawasilisho ya maoni kutoka kwa watendaji na watunga sera, na pia watafiti wanaofanya kazi na jamii hizi, kujadili njia zinazowezekana za kazi katika sehemu za wasomi, tasnia, sekta ya umma, na mashirika yasio ya serikali. Mawasilisho yanaweza pia kujumuisha masomo kutoka kwenye juhudi za kuunganisha utafiti na utendaji kazi.

 • Shida Zilizopatikana kwa njia ya ripoti za taarifa zinazoelezea shida zinazojitokeza katika utendaji zinazoathiri jamii ambazo hazijapata huduma bora na zilizotengwa. Shida zinapaswa kuwa zile zinazofaidika na umakini mpana ndani ya jamii ya watafiti. Mawasilisho yanapaswa kutoa habari ya msingi juu ya shida, muhtasari wa njia yoyote iliyopo au njia za kushughulikia shida husika, na majadiliano juu ya jinsi mbinu kutoka kwenye mifumo, taratibu na ufikiaji wa hesabu za biashara zinavyoweza kuchangia suluhisho. Pia, mawasilisho yanahimizwa kutoa mjadala wa changamoto katika kutoa suluhisho kamili, kushiriki maono kutoka kwenye ushirikiano kati ya wasomi na watendaji, na/au kuanzisha njia mpya za kushughulikia shida iliyopo.

 • Nyaraka za uchunguzi ambazo hutoa muhtasari mpana wa mada fulani ya umuhimu wa mkutano huo. Uwasilishaji unapaswa kuchunguza kazi inayofaa kwenye eneo hili na uwasilishwe kwa njia kamili na ya mshikamano. Mbali na tafiti za kina, pia tunatia moyo sana mawasilisho ya maoni kutoka kwa watunga sera na watendaji ambao wanachunguza njia za kisasa zinazotumiwa katika sehemu fulani kuu ya programu na zinaweza kupatikana mbele ya hadhira ya wasomi na isio ya kitaaluma.

Maelekezo ya Uwasilishaji

Kwa ufuatiliaji wa utafiti, mawasilisho yatakuwa na chaguo la kuwa ni ya kumbukumbu au isio ya kumbukumbu, na upendeleo uliopewa kuwa nyaraka za kumbukumbu. Ufuatiliaji wa kumbukumbu unakaribisha mawasilisho ambayo yanajumuisha nyaraka mpya za utafiti ambazo hazijachapishwa katika maendelezi ya kongamano hapo awali. Ufuatiliaji wa kumbukumbu unakaribisha nyaraka ambazo ziko kwenye utaratibu wa kuchapishwa kwenye majarida. Ufuatiliaji ambao sio wa kumbukumbu pia unakaribisha nyaraka za utafiti ambazo hazijachapishwa mapema kuzidi mwezi Januari mwaka 2020. Waandishi wanapaswa kupakia PDF ya utafiti wao kwenye EasyChair. Hakuna mahitaji ya upangiliaji au urefu wa uwasilishaji wa nyaraka ya mfumo wa PDF, lakini nyaraka zilizokubalika zitakuwa na kikomo cha kurasa 14 wakati wa kuchapishwa kwa kutumia kiolezo hiki husika cha ACM. Mbali na mfumo wa PDF, waandishi wanatakiwa kupakia maelezo yenye maneno 200-250 kwenye EasyChair kwa muhtasari wa kile walichokiwasilisha na umuhimu wake kwenye kongamano hilo.

Mawasilisho yanafanywa bila ya kujua ni nani ambaye amehusika nayo: waandishi wanapaswa kuchukua tahadhari wasijumuishe majina na ushirika wa waandishi kwenye karatasi zao, pamoja na wakati wa kutaja kazi ya awali. Wawasilishaji wanapaswa kuorodhesha waandishi wote wenza juu ya kazi iliyowasilishwa katika EasyChair lakini sio kwenye mfumo wa PDF ya uwasilishaji.

Kutakuwa na chaguo la kuchagua kati ya kutunza kumbukumbu (kwa zile zilizochapishwa) au zisizo za kumbukumbu (ambazo hazikuchapishwa). Waandishi wanaweza kuwasilisha kazi ambazo hazijachapishwa, kazi inayopitiwa kabla ya kuwasilishwa, au kazi ambayo imechapishwa mapema zaidi ya Januari ya mwaka 2020. Ikiwa kazi hiyo tayari imechapishwa, tafadhali jumuisha nukuu kwenye EasyChair.

Tutakubali tu mawasilisho kwa lugha ya Kiingereza. MD4SG na EEAMO wamejitolea kwa kukuza jamii za lugha nyingi, na tunatarajia kuruhusu mawasilisho katika lugha zingine kwenye matukio yajayo.

Mapitio

Mawasilisho yatafanyiwa tathmini kwa kuzingatia vigezo hivi vifuatavyo:

 • Ubora wa uwasilishaji unaopimwa kwa usahihi na uwazi wa ufafanuzi.
 • Umuhimu kwa lengo la kongamano.
 • Uwasilishaji wa tukio jipya na halisi linalowezekana: tunahimiza sana kazi ambayo inachunguza matumizi ya tukio halisi linalowezekana au hutumia mbinu za matendo mapya yanayowezekana kusoma matukio ya programu zilizopo.
 • Pia, mawasilisho yatatathminiwa kulingana na:
  • Uwezo wa kazi ya ufuatiliaji wa taaluma mbalimbali. Tunakaribisha mawasilisho yenye uwezo wa kuchochea ushirikiano kati ya taaluma mbalimbali,
  • Uwasilishaji wa maarifa maalum ya eneo. Tunakaribisha haswa watendaji walio na hamu au uzoefu katika kutafsiri kati ya shida za kiutendaji na njia za utafiti wa kitaaluma.

Nyaraka ambazo ziko nje ya mtazamo wa kongamano kama zilivyotathminiwa na vigezo hivi zinaweza kukataliwa kushiriki.

EAAMO’22 itafuata mfumo wa ukaguzi wa awamu mbili. Mawasilisho yote yatakaguliwa na watu wa kada moja ambapo ni angalau wahakiki 2 katika muundo wa kutojua wanahakiki kazi ya nani hasa. Kamati ina haki ya kutopitia maelezo yote ya kiufundi ya maoni ya mawasilisho.

Baada ya mapitio kukamilika, wasilisho litakubaliwa lilivyo, kukataliwa au kukubaliwa kwa sharti la kuwasilisha masahihisho husika. Ikiwa inabidi kufanya masahihisho, wahusika watapewa takribani wiki 3 kama tarehe zinavyonyesha hapo chini kukamilisha masahihisho. Kipindi hicho, ‘mshauri’ atateuliwa kwa kila wasilisho kuhakiki masahisho husika. Halaf wasilisho litakubaliwa na kupelekwa hatua za mbele kwa mwenyekiti wa eneo la kitaalam na program kwa uamuzi wa mwisho.

Mawasilisho ambayo hayatakubaliwa kama nyaraka kamili zitawasilishwa kuandaa wasilisho la bango wakati wa kongamano. Mabango yatawasilishwa kwa jamii nzima wakati wa kongamano ila hayataingia katika machapisho ya mwisho.

Msaada wa Kifedha

Kongamano hili litatoa msaada wa kifedha kwa gharama za usajili na usafiri, pamoja na bando la mtandao kama kongamano litafanyika kwa njia ya mtandao. Maombi yote ya msaada wa kifedha lazima yawasilishwe ifikapo tarehe 20 Aprili, 2022 (kokote duniani); maombi yaliyopokelewa baada ya tarehe hii hayatazingatiwa. Taarifa zaidi kuhusu mfumo wa kuomba msaada kwa kifedha zitatolewa siku za usoni.

Taarifa za muhimu

 • Tarehe ya Mwisho ya Kuwasilisha Utafiti: 20 Aprili 2022, Kokote Duniani
 • Ukurasa wa Kuwasilishia Utafiti: EasyChair
 • Tarehe ya mwisho wa Maombi ya Msaada wa Kifedha: 20 Aprili 2022, AoE
 • Siku ya Kujulishwa: Mwisho wa mwezi Juni 2022
 • Tarehe za Tukio: 6-9 October 2022